KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani > Tunatafuta wasambazji wapya na wakusanyaji wapya wa mbegu

Tunatafuta wasambazji wapya na wakusanyaji wapya wa mbegu. Jiunge kwenye mtandao wa KPR wa wasambazaji na wakusanyaji wa mbegu!

1. jinsi ya kuwa msambazaji wetu wa mbegu

Kama wewe ni msambazji wa mbegu tayari au mzalishaji wa mbegu, tunapenda kushirikiana nawe. Tunakisia kwamba tayari unafahamu jinsi ya kuvuna mbegu, jinsi ya kuzisafisha na kuzihifadhi, hivyo hatuhitajiki kukueleza jinsi ya kufanya hivyo. Hata hivyo, kama una maswali yoyote au wasiwasi, tutafurahi kukusaidia.

Tunafanyakazi kuliangana na utaratibu ufuatao:

Tutumie orodha ya bei ya mbegu zako katika Euro au Dola za Marekani ( au katika fedha yoyote ile). Angalia mfano. Bei kwa mbegu kwa kawaida inaonyoshwa bila ya gharama za usafirishaji. Gharama za usafirishaji zinatozwa zaidi wakati wa kusafrisha mbegu.

Tunavutiwa na mimea yoyote kutoka kwenye eneo lako - mimea ya mapambo, mime ya vyakula (matunda na mboga za majani), mimea ya madawa, mimea isiyoelezeka, mimea ya kiufundi (kwa kuzalishaji wa nguo, ujenzi wa nyumba nk) na mimea ya porini.

Kumjaribu msambazaji mpya wa mbegu

Tunapoanza mahusiano mapya ya kibiashara na msambazaji mpya wa mbegu, tunamhitaji yeye kutuma kwanza kwa shehena ya majaribio. Kama tutaona kutu kinachovutia katika orodha yako ya mbegu, tutaweka oda ya majaribio. Kuepuka udanganyifu hatulipi kwa shehena ya kwanza kabla ya kupokea na mbegu kujaribiwa. Mahitaji ya wanachama wetu na wateja ni makubwa; hivyo tunahitaji kuwa na uhakika kwamba mbegu unazotoa ziko katika kiwango cha juu. Mara tu tunapopokea shehena ya majaribio kutoka kwako, tunazijaribu mbegu ulizosambaza (jaribio la uotaji, kuangalia kama mbegu zilizotumwa ni kweli spishi zake zinazotambulika).

Hii shehena ya kwanza ni ya muhimu sana, kwasababu kama mbegu zako zitafaulu majaribio yetu, unaweza kufurahia mahusiano ya muda mrefu ya kibaisha na sisi. Hata hivyo, kama mbegu zako zinashisnwa majariibio yetu, hatutalipia shehena hiyo na hatutaweza kufanya biashara yoyote na wewe. Hata hivyo kama mbegu zako zitafaulu majaribio yetu, tutalipia mebgu pamoja na gharama za usafirishaji, lakini hatutalipa kitu chochote kama hazikufaulu majaribio yetu.

Tafadhali tuma mbegu mpya na zinazoweza kupatikana. Kuzuia kuharibika kwa mbegu kutokana na unyevunyevu, tunashauri kwamba usifungashe mbegu zako kwenye mfuko wa plastiki. Njia mzuri ni kufungasha kwenye mfiuko wa karatasi. Cheti cha ubora wa mimea kwa kawaida hakihitajiki (tutakujulisha tutakapoweka oda na wewe). Tutakubaliana na njia za usafirishaji tutakapoweka oda na wewe.

Tunapenda kukujulisha, kuwa msimu wa uoto Ulaya (ambako wanachama na wateja wengi wa KPR wanaishi) unaaza Aprili – Mei na kumalizika Septemba – Oktoba. Mbegu nyingi Ulaya zinavunwa hadi mwishoni mwa Septemba. Oktoba – Novemba, tunachapisha katalogi ya mbegu mpya tunazotoa. Idadi kubwa ya wanachama wetu wananunua mbegu kutoka kwetu kuanzia Oktoba hadi Januari ( nawakati mwingine hadi Machi), kwasababu wanataka mbegu ziwe mikononi mwao kabla ya msimu mpya wa uoto kuanza, inamaana kwamba mbegu zinapaswa kupandwa Machi mapema, ili mimea isyostahimili baridi inaweza kukuwa wakati wa msimu wa jua kukuwa na hali nzuri ya hewa. Msimu wa baridi Ulaya ni kuanzia Novemba hadi Machi na nchi za Ulaya, mimea ya kitopika inatakiwa kuhifadhiwa ndani ya nyumba, maana itauwawa na baridi ikiwekwa nje.

2. jinsi ya kuwa mkusanyaji wetu wa mbegu

Huhitaji kuwa mwanabotania kufanyakazi na sisi. Wanasayansi ulimwenguni mara nyingi wanatafuta mbegu za mimea inayotambulika kwa urahisi, ambayo inaweza kutambuliwa na mtu yoyote bila matatizo yoyote. Mimea hii haihitaji kuwa adimu, na mara nyingi inatokea kw ukubwa kwenye eneo, lakini wanahitaji mimea hii kwaajili ya utafiti zaidi (sampuli zaidi za spishi moja kutoka kwenye nchi nyingi tofauti iwezekanavyo na kutoka kwenye maeneo mengi tofauti (wuwingi) katika nchi moja iwezekanavyo). Wakati mwingine baadhi ya mimea hii, inahitajiwa na mtu duniani, kuza kwenye bustani yako kama magugu. Inawezekana pia mahali Fulani kwenye mji wako, au karibu na nyumba yako, spishi nyingi za mimea inayohitajika inakua!

Kutokana na ukweli kwamba mahitaji kw (hasa porini) spishi za mimea iliyokusanywa ni ya hali ya juu, na hakuna mtu mwenye bidhaa za kiwango hicho kama KPR, hatuwezi kukidhi mahitaji yote. Kwa hiyo, tunatazamia washirika wapya Afrika, Asia, Marekani, Australia na Oshenia. Asante kwa ukweli kwamba tunapunguza gharama zetu za usafirishaji, tunaweza pia kupunguza bei. Gharama zako za kusafiri hakika zitakuwa chini zaidi kama tutafanya safari kama hiyo kutoka Slovakia. Wakati mwingine gharama zako za kusafiri hazihitajiki, kama baadhi ya mbegu zinazohitajika zinaweza kukusanywa kutoka ndani ya eneo la nyumbani kwako, sehemu yako ya kazi au eneo lingine la jirani. Unaweza pia kukusanya mbegu wakatika ukiwa mapumzikoni kwenye nchi yako (labda kwenye maeneo ya pwani au nchi kavu au kwenye milima – uwezekano hauna mwisho!

Jinsi gani uwe mkusanyaji mbegu wa KPR?

Kama unapenda kushiriki kama mmoja wa wakusanyaji wetu wa mbegu, unakaribishwa san! Taaluma yako siyo muhimu kabisa! Jambo la pekee la muhimu ni kwamba unaifahamu mimea ambayo utakuwa ukivuna mbegu. Kwa upande mwingine, kama ni mwanabotania au mtu fulani mwenye ufahamu mzuri wa mimea, hii ni dhahiri kwamba ni faida. Wakati wote kusanya mbegu ambazo unafahamu majina yake ya kilatini, na ambayo una uhakika nayo kwa 100%. Kama huna uhakikia kwa 100% ya majina sahihi, unaweza pia kuchukua foto ya mmea, kabla ya kututumia.

Mara tu utakapojiunga kwenye mtandao wetu, tutakutumia “Orodha yetu inayotakiwa” ya sasa katika utaratibu wa kawaida, lakini huzuiwi kusambaza kitu chochote. Unakaribishwa kusambaza spishi zinazopatikana kwako kwa urahisi, hata hivyo kama umeshindwa kusambaza kitu chochote siyo tatizo.

Kwasababu hatujui sheria za nchi yako, maana hatuko chini kwako, tunaomba usikusanye mbegu za mimea ambayo imezuiwa kwa mujibu wa sheria za nchi yako. Tafadhali usivunje sheria za nchi yako! Tafadhali usikusanye spishi zilizozuiwa hata kama zimeonyshwa kwenye “Orodha yetu inayotakiwa”. Katika baadhi ya nchi, baadhi ya spishi inaweza kuwa ya kawaida na haizuiwi na sheria, wakati kwenye nchi zingine, spishi hiyo hiyo inaweza kuwa adimu sana au haipatikani kabisa. Hatuwezi kubadilisha “Orodha yetu inayotakiwa” kwa kila nchi, hivyo tunategeme wewe kuhusika na suala hili.

Usikusanye mbegu kutoka kwenye memea wowote kutoka kwenye viunga vua kifamilia, kasababu hatushughuliki na viunga.

Unaweza aidha kukusanya mbegu kutoka kwenye mimea iliyotajwa kwenye “Orodha yetu inayotakiwa” tu au unaweza kututumia orodha ya mimea ambayo unaweza kukusanya mbegu. Baada ya kupokea orodha yako, tutakutumia barua pepe ya orodha ya mbegu tulizovutiwa nazo.

Tunavutiwa na mimea yoyote kutoka kwenye eneo lako - mimea ya mapambo, mime ya vyakula (matunda na mboga za majani), mimea ya madawa, mimea isiyoelezeka, mimea ya kiufundi (kwa kuzalishaji wa nguo, ujenzi wa nyumba nk) na mimea ya porini.

Ubora gani nikusanye na kwa namna gani?

Ni vigumu kueleza, kwasababu wakati mwingine unaweza kuvuna mbegu 50 – 1000 au hata zaidi kwa sekunde chache kwa kutoa mbegu kutoka kwenye matunda. Katika kesi nyinge hata hivyo, inaweza kuchukua masaa kukusanya japo mebgu 100. kusanya angalau mebgu 100 kwa mahali, lakini kama inawezekana, tafadhali kusanya saidi ya (500 – 1000). Kama kuna mmea mmoja tu unaopatikana mahali fulani kwa mfano, kusanya mbegu 10, 20, 50….tu – tunashukuru kwa kiwango chochote utakachoweza kusambaza. Kwa kawaida inatosha kukusanya hadi mbegu 100 – 200 za mbegu kubwa (kubwa zaidi ya sm 3). Kama unawasi wasi wowote, tafadhali jisikie huru kuwasiliana nasi wakati wowote na shaurina nasi.

Tafadhali kumbuka wakati wote kuacha mbegu wakati unapokusanya mbegu, kuepuka kupotea kwa mmea.

Kama mimea zidi inapatikana katika eneo moja, kusanya mbegu kutoka katika kila mmea iwezekanavyo, ili sampuli ya mbegu zako iwakilishe jenetiki inayopatikana (utofauti wakibaiolojia) wa mimea katika eneo husika

Kama unaweza kukusanya spishi za iana moja kutoka kwenye eneo la asili zaidi ya moja, kusanya kutoka kwenye meneo ya asili mengi tofauti iwezekanavyo. Kutambua maenep ya asili tofauti si rahici hivyo - zingatia eneo kama mahali ambapo mimea kutoka eneo lingine haihusiani moja kwa moja na mimea hiyo. (Mf. uwezo wa kuzaa (Mf. Sedum, Sempervivum, au mimea mingine yoyote)

Kama uko kwenye eneo ambalo unaweza kukusanya spishi zaidi, hata kama hazikutajwa kwenye “orodha yetu inayotakiwa” tafadhali kusanya (tutaziweka kwenye benki ya mbegu na karibuni au baadaye mtu taihitaji). Unaweza pia kututumia ordha ya spishi ambazo unaweza kukusanya na ambazo hazipo kwenye “Orodha yetu Inayotakiwa” au katika kusanyiko letu la mbegu kwenye Benki yetu ya Mbegu na Mimea” au spishi ambazo hazikutajwa kwenye Benki yetu ya Mbegu na Mimea: kutoka kwenye nchi yako. Tutakutumia barua pepe ya taarifa kuhusu spishi gani tulizovutiwa nazo. Tutashukuru kama utaweza kukusanya.

Kama unakusanya mbegu kutoka porini (siyo mbegu zilizokusanywa kwenye mimea ambayo haijulikani uasili wake (kwenye bustabi)), Tafadhali andika wazi taarifa zifuatazo kwenye karatasi ya begi unalosafirishia mbegu zako.

Lazima inahitajika:

- jina la Kilatini la mmea
- mahali halisi ilipokusanywa, vile vile maelezo mafupi ya tabia (konde la majani, mchanga, mwambao mwa bahari, miteremeko, miamba, milima, nk) – tafadhali hakikisha kwamba da ziko zinakuwa za undani iwezekenavyo ili kwa mtu yeyote aweze kutafuta mbegu hizo, hata katika matukio ambayo hayakutokea nchini kwako kabla. (angalia sampuli)
- jina la nchi yako
- tarehe ya ukusanyaji (katika fomati ya tarehe – mwezi – mwaka)
- simbo yako ya utambulisho ambayo itatolewa kwako au jina lako kamili

Taarfa za ziada zinakaribishwa, lakini siyo lazima:

- eneo kwa mujibu wa GPS (kama una GPS)
- taarifa zingine zozote

Tunashauri sana matumizi ya mabegi ya karatasi zaidi kuliko mabegi ya plastiki kusafirishia mbegu, kwa sababu unyevunyevu ndani ya mfuko wa plastiki unaadhiri sana mbegu. Weak mbegu kwenye mfuko wa karatasi kwenye sehemu kavu mbali na mwanga wa jua (mf. katika boksi gumu)

Vipi kuhusu mbegu za metunda ya maji maji kama matunda madogo

Wakati mwingine ni heri kuacha tunda likauke, ili uondoe mbegu kutoka kwenye tunda lililokauka kwa urahisi. Katika kesi zingine, ni bore kuweka tunda kwenye maji kwa saa hadi siku moja na mara kwa mara osha tunda lililoharibika, hadi mbegu iweze kuchukuliwa kutoka chini ya tunda. Kisha iache ikauke na fungasha kwenye mfuko wa karatasi.

Kwa baadhi ya spishi (mf. ulimaji wa asili wa miti inayolika, mebgu – hazizalishwi Allium) siyo mizuri kwa kuzalisha mbegu, lakini ni bora kuzitoa kama matunguu vipandikizi au sehemu yoyote yam mea. Kwa kesi hii tafadhali wasiliana nasi na tutajadili maelezo yake kwanza.

Mara tu utakapokuwa na mbegu unazopenda kusambaza kwentu, tafadhali tutumie barua pepe na orodha ya spishi zilizopo (safu fomula hapa). Unakaribishwa kututumia orodha mara moja kwa mwaka baada ya msimu maalum, au kila wakati unapokusanya mbegu mpya. Wakati muafaka wa kututumia orodha hata hivyo ni kabla ya Septemba ya kila mwaka. Kama kwa namna yoyote ile unavuna mbegu baada ya Septemba, tafadhali bado tutumime orodha. Kwa upande mwingine , mebgu zote zinazovunwa kabla ya Septemba, ziwekwe kwenye orodha na tutumie. Mara tu tutakapopokea orodha yako, tutakujulisha iwapo utume kitu chochote haraka au baadaye.

Napenda kujiunga na mtandao wa KPR kama msambazaji mbegu/ mkusanyaji mbegu

Tafadhali nipatie maelezo mafupi kwa Kiingereza kuhusu wewe na ufahamu wako wa mimea na pia uzoefu wako.

Taarifa muhimu kwa marafiki walio nje ya Ulaya (Umoja wa Ulaya)

Kuna mipaka kidogo ya uuzaji wa mimea ulimwenguni kama vile Ulaya. Nchi nyingi duniani zimesaini makubaliano ya CITES (makubaliano ya kimataifa ya uuzaji wa spishi zilizohatarini). Hii ni orodha ya mimea (na wanyama) ambayo uuzaji wake umezuiwa au imewekewa mipaka.

Umoja wa Ulaya umesaini makubaliano hayo pia, lakini pia unasheria zake, ambayo ni kali zaidi ya CITES (mf. Commission Regulation (EC) No 338/1997). Sheria za Umoja wa Ulaya zinafunganisha nchi zote za Umoja wa Ulaya. Kuna vipengele 4 (A, B,C na D sawa na CITIES)

Orodha ya spishi katika kila kipengele ni sawa na vipengele vilivyomo kwenye CITIES, lakini soyo sawa wakati wote. Baadhi ya spichi zimeorodheshwa kwenye kipengele kingine na kuna spishi nyinge ambazo hazikutajwa kwenye vipengele vya CITES. Kwa kuongezea hapa, Umoja wa Ulaya mara nyingi hutoa sheria ambapo baadhi ya spishi muhimu inazuiwa kwa muda kwenye Umoja wa Ulaya.

Tunaelewa kwamba huwezi kujua mipaka yote ya Umoja wa Ulaya, na hivyo tumeandaa orodha ya mimea kwa manufaa yako, ambayo hatuvutiwi nayo. Safu hapa.

Usitupatie spishi yoyote ilitozuiwa kutoka nchini kwako!