KPR - Klabu ya Wakulima wa Bustani

KPR ilianzishwa rasmi mwaka 2000 huko Slovakia, Ulaya; hata hivyo tunasambaza mbegu na mimea dunaiani kote tangu mwaka 1998.

Dhumuni letu kuu ni kuwaunganisha wakulima wa bustani dunia nzima kutoka kwenye mashamba yote ya kuvutia ili kutengeneza hifadhidata kubwa ya mbegu na mimea (Benki ya Mbegu na Mimea ya KPR).

Kwasasa tuna matawi makubwa 6 (Slovakia, Ucheki, Australia, Uhindi, Tailandi, Afrika ya Kusini na Tanzania) na washirika na wakusanya mbegu zaidi ya 300 duniani kote.

Siku hizi tunaweza kukusanya na kusambaza spishi za mimea zaidi ya 10,000 duniani kote.

Kama unatafuta kitu chochote, uko mahali sahihi! Ingawa bado hatuna kila mmea katika kusanyiko letu, lakini tunakua kila siku, hatua kwa hatua, mbegu kwa mbegu, mmea kwa mmea. Tunaamini kwamba karibuni tutaweza kusambaza karibu kila kitu!